Karibu 400 wanahitaji matibabu Madaya

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watu waliozingirwa mji wa Madaya

Mkuu wa huduma za kibinadamu katika umoja wa mataifa anasema kuwa karibu watu 400 waliozingirwa katika mji wa Madaya nchini Syria wanahitajika kuondolewa mjini humo kwa dharuara ili kupata matibabu .

Stephen O'Brien alitayasema hayo baada ya mkutano wa baraza kuu la umoja wa mataifa uliofanyika kujadili hali katika mji huo unaodhibitiwa na waasi karibu na mji wa Damascus.

Mapema msafara wa malori ya misaada ulipeleka tani 40,000 kwa wenyeji ambao wamezigirwa na serikali kwa miezi kadha.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Magari ya umoja wa mataifa yakipeleka misaada Madaya

Umoja wa mataifa unasema kuwa umapata ripoti kuwa watu wanakufa kutokana na njaa.

Msaada wa siku ya Jumapili ndio wa kwanza kuruhusiwa kuingia katika mji wa Madaya tangu mwezi Oktoba wakati shirika la mpango wa chakula la umoja wa mataifa lilipeleka msaada wa mwezi mzima kwa watu 20,000.

Pia magari yaliyobeba misaada yaliingia miji miwili inayozingirwa na waasi katika mkoa wa kaskazini wa Idlib chini ya makubaliano kati ya pande zinazopigana.