Charles Rwomushana aachiliwa

Image caption Rwomushana alikamatwa baada ya maoni yake kuhusu kukamatwa na labda kuuawa kwa Chris Aine

Aliyekuwa jasusi nchini Uganda Charles Rwomushana ameachiliwa kutoka kuzuizi cha polisi.

Aliripotiwa kutoweka mwishoni mwa wiki na kulikuwa na uvumi kuwa alikuwa mikononi mwa kitengo ya ujasusi cha nchi hiyo.

Lakini polisi wamekana kumuzuilia. Inaripotiwa kuwa bwana Rwomushana alishikwa na polisi ambao walikuwa wamevalia kiraia siku ya Ijumaa wakati alikuwa njiani kuhudhuria mahojiano katika kituo kimoja cha runinga .

Bwana Rwomushana alikamatwa baada ya maoni yake kuhusu kukamatwa na labda kuuawa kwa Chris Aine ambaye ni mkuu wa ulinzi wa mgombea urais Amama Mbabazi.