Watu 10 wauawa katika mlipuko Uturuki

Haki miliki ya picha DHA
Image caption Polisi washika doria katika eneo la mlipuko Uturuki

Mlipuko mkubwa umetokea katika mji mkuu wa Uturuki, Istanbul.

Mlipuko huo umetokea katikati mwa mji wa kale wa Istanbul.

Eneo hilo huwa kivutio kikuu cha watalii.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mlipuko karibu na msikiti Uturuki

Maafisa wa polisi kwa sasa wamedhibiti eneo hilo.

Afisi ya gavana wa Istanbul inasema kuwa watu kumi wameuwawa na 15 kujeruhiwa.

Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa zasema kuwa ni shambulizi la kujitoa muhanga.