Hong kong kudhibiti uwindaji haramu

C Y LEUNG Haki miliki ya picha GETTY IMAGES
Image caption Kiongozi mkuu wa Hong Kong C Y LEUNG

Kiongozi mkuu wa Hong Kong , C Y Leung, anasema serikali yake ina hofu kubwa kuhusu biashara haramu ya pembe za ndovu kutoka mataifa ya Afrika, na kwamba itaanzisha sheria mpya na kali za kukabiliana na biashara ya pembe za ndovu.

Bwana Leung amesema Hong Kong itapiga marufuku uagizaji na ununuzi wa bidhaa zinazotengenezwa kutokana na pembe za ndovu.

Aidha amesema serikali yake itaangalia uwezekano wa kuchukuliwa kwa hatua nyingine ikiwemo kuweka masharti ya biashara ya pembe za ndovu, na kuweka faini nzito kwa wizi wa viumbe waliomo wanaokabiliwa na hatari.

Haki miliki ya picha BBC Chinese
Image caption Hong Kong imekua soko la pembe haram za ndovu kutoka Afrika

Mji wa Hong Kong ni miongoni mwa vituo muhimu vya biashara ya pembe za ndovu zinazosafirishwa huko baada ya kuuawa kwa ndovu kutoka mataifa ya Afrika ikiwemo Tanzania, kenya na Zimbabwe.

Licha ya kupigwa marufuku na mataifa biashara haramu ya pembe za ndovu imesababisha kupungua kwa idadi ya wanyama hao kwenye baadhi ya mbuga za wanyama barani Afrika, jambo linalotia hofu ya kutoweka kabisa kwa viumbe hao iwapo biashara hiyo itaendelea.