Kikosi cha UN hakitazima ghasia Burundi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Baraza la usalama la umoja wa mataifa

Ujumbe wa kisiri uliotumwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na afisa wa umoja huo unaonya kuwa kikosi cha kulinda amani ambacho kinapangiwa kutumwa kwenda nchini Burundi huenda kikashindwa kuzima ghasia katika nchi hiyo inayokumbwa na mzozo.

Ujumbe huo uliotumwa na mkuu wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa unalishauri baraza hilo kutuma wanachama wake kwenda nchini Burundi kwa mazungumzo ya dharura kuhusu mzozo huo uliosababishwa na hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu.

Burundi imekuwa ikishuhudia ghasia zaidi tangu Nkurunziza atangaze nia yake ya kugombea urais. Baadaye alishinda uchaguzi huo.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mamia ya watu wameuawa kwenye ghasia nchini Burundi

Mamia wameuawa na maelfu ya watu wamekimbilia nchi majirani wakihofia kutokea kwa vita kamili.

Burundi imekataa kikosi kilichopendekezwa cha wanajeshi 5000 kutoka kwa Muungano wa Afrika kuzima ghasia, ikiitaja hatua hiyo kama uvamizi wa kijeshi.