Hatari ya kuwasiliana ukiwa kazini

Image caption Muajiri ana haki ya kufuatilia mawasiliano ya wafanyikazi

Waajiri wanaweza kusoma mawasiliano ya mwajiriwa ambayo hufanywa wakati wa kazi.

Mahakama ya haki kibinadamu ya bara Ulaya imesema kuwa kampuni iliyosoma mawasiliano ya mfanyikazi katika mtandao wa Yahoo Messenger akiwa kazini ilikuwa na haki ya kufanya hivyo.

Mfanyikazi huyo ambaye ni mhandisi nchini Romania alikuwa na matumaini kuwa mahakama ingeamua kuwa muajiri wake alikuwa amekiuka haki zake wakati alisoma ujumbe wake na kumfuta kazi mwaka 2007.

Mwanamume huyo Bogdan Barbulescu alikuwa ameshindwa kwenye kesi katika mahakama za Romania, na alikata rufaa kwa mahakama ya haki za binadamu ya Ulaya.

Majaji walisema kuwa mfanyikazi alikuwa amekiuka sheria za kampuni kwa kufanya mambo ya kibinafsi saa za kazi na hivyo basi kampuni ilikuwa na haki ya kufuatilia shughuli zake.

Hata hivyo, imesema sera kama hizo pia ni lazima ziwalinde wafanyikazi dhidi ya uchunguzi usiohitajika.

Haki miliki ya picha apps
Image caption mitandao ya mawasiliano

Majaji hao katika mahakama ya haki za binadamu ya bara ulaya mjini Strasbourg walitoa uamuzi wao siku ya Jumanne.

Inajumuisha nchi zote zilizotia sahihi makubaliano ya haki za binadamu ya Ulaya ikiwemo Uingereza.