Mauzo Kutoka Afrika yalishuka China

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mahitaji ya bidhaa kutoka afrika kama vile mafuta, madini na vyuma imepungua kwa kiasi kikubwa

Maafisa wa idara ya forodha nchini Uchina wamesema kuwa mauzo kutoka bara la Afrika nchini humo yalishuka kwa asilimia 40 mwaka uliopita.

Uchina ndilo soko kubwa zaidi ya bidhaa kutoka Afrika na kuongezeka kwa mahitaji ya bidhaa za Afrika kumeimarisha ukuaji wa uchumi barani Afrika.

Kupungua kwa mauzo kunaashiria jinsi uchumi wa Uchina ulivyokwama katika siku za hivi karibuni.

Hali hii imefanya uchumi wa Afrika kudorora na ndio maana dhamani ya safari ya nchi nyingi imeshuka.

Haki miliki ya picha
Image caption Dhahabu kutoka Afrika

Akitoa takwimu za mwaka uliopita za biashara nchini Uchina, msemaji wa idara ya forodha Huang Songping amewaambia waandishi wa habari kuwa mauzo kutoka Afrika kwa ujumla ilikuwa dola billioni 67, kiwango ambacho ni asilimia 38 chini ya ilivyokuwa mwaka wa 2014.

Mwandishi wa BBC wa masuala ya biashara amesema kuwa uchumi wa Uchina unaelekea kukumbana na wakati mgumu na wachanganuzi wa masuala ya uchumi wanasema mahitaji ya bidhaa kutoka afrika kama vile mafuta, madini na vyuma imepungua kwa kiasi kikubwa na hivyo kupunguza bei ya bidhaa hizo.

Aidha ni kiwango kidogo to fedha zinazotoka Uchina kuingia barani Afrika imepungua.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Soko la hisa nchini China

Uwekezaji kutoka Uchina ulipungua kwa asilimia 40 katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mwaka wa 2015.

Huku hayo yakijiri, mahitaji ya bidhaa za Uchina barani Afrika imeendelea kuongezeka.

Mwaka wa 2015 Uchina iliiuza bidhaa za dola bilioni 102 barani Afrika kiwango ambacho ni ongezeka la asilimia 3.6.

Mwaka uliopita Afrika Kusini iliandaa mkutano wa biashara ulioleta pamoja mataifa ya Afrika na Uchina ambapo rais wa Uchina Xi Jinping alitangaza msaada wa dola bilioni 60 kwa mataifa ya Afrika.