Watu watatu wajishindia dola bilioni 1.5

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Washindi watagawana zawadi ya dola bilioni 1.5. Wanaweza kupata malipo kila mwaka kwa miaka 29 au walipwe kitita chote cha dola millioni 930.

Kuna takriban tikiti tatu za ushindi kwenye mchezo wa bahati nasibu unafahamika kama Powerball Lottery nchini Marekani wa dola billioni 1.5.

Tikiti zilizoshinda mchezo huo unafahamika kama Powerball Jackpot ziliuzwa katika majimbo la Carlifonia, Tennessee na Florida.

Watu walioshinda mchezo huo bado hawajulikani.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Maelfu ya watu walipanga milolongo kununua tikiti

Maelfu ya watu walipanga milolongo mirefu nje ya maduka kote nchini marekani kununua tikiti.

Tikiti ya ushindi iliuzwa katika jimbo la Carlifonia kwenye kitongoji cha Chino Hills. Picha za televisheni zilionyesha umati ukisherehekea katika duka wakati matokeo yalipotangazwa .

Washindi watagawana zawadi ya dola bilioni 1.5. Wanaweza kupata malipo kila mwaka kwa miaka 29 au walipwe kitita chote cha dola millioni 930.