Familia ya Savimbi Kushtaki

Image caption Wakili kwa mchapishaji wa video hiyo anasema kuwa Savimbi anawakilisha jinsi alivyokuwa mkuu wa waasi ambaye alipigana na MPLA

Kumeibuka ripoti kuwa familia ya kiongozi wa zamani wa waasi wa Unita Jonas Savimbi inashtaki kuhusu kuhusishwa kwake katika mchezo wa video kwa jina Black Ops II.

Savimbi anaonekana kwenye mchezo huo akiongoza kikosi cha Unita kwenye vita dhidi ya wapiganaji wa MPLA mwaka 1986.

Katika video hiyo Savimbi anawashauri watu wake kusonga mbele vitani na kupigana akisema kwa sauti "kifo kwa MPLA."

Mwishoni Savimbi anaweza kusikika akicheka na kujigamba kuhusu ni wapiganaji wangapi wa MPLA waliouawa.

Etienne Kowalski, wakili kwa mchapishaji wa video hiyo anasema kuwa Savimbi anawakilisha jinsi alivyokuwa mkuu wa waasi ambaye alipigana na MPLA.