Whatsapp na viber kudhibitiwa AK

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Whatasap ina watumiaji Zaidi ya milioni kumi nchini Afrika Kusini

Mitandao ya whatsapp na viber huenda ikadhibitiwa Afrika Kusini ikitegemea matokeo ya vikao vya bunge baadaye mwezi huu, umeripoti mtandao unaoheshimika wa Fin24.

Umaarufu wa Whatasap inayomilikiwa na facebook umeongezeka nchini Afrika Kusini ukiwa na watumiaji Zaidi ya milioni kumi kwa mujibu wa ripoti ya World Wide Worx na Fuseware.

Kampuni mbili kubwa za simu Afrika kusini Vodacom na MTN mwaka uliopita zilitoa wito wa kudhibitiwa kwa huduma hizo.

Haki miliki ya picha no credit
Image caption Mtandao wa Viber

"Kuna hawa washiriki wanaopata manufaa makubwa katika sekta hii bila kutumia pesa. Tutapataje usawa?" afisa mmoja wa MTN alinukuliwa akisema.

Kamati ya bunge kuhusu mawasiliano ya posta ilipanga kufanya kikao hicho tarehe 26 mwezi January kujadili sera za kuingilia kati swala hilo.