Waliohukumiwa kifo walalamika Zimbabwe

Image caption Mara ya mwisho mfungwa kunyongwa nchini Zimbabwe ilikuwa 2005

Kiongozi wa mashtaka nchini Zimbabwe amesema kuwa taifa hilo halijakuwa likifanya hukumu ya kifo kwa sababu halina mfanyikazi wa kunyonga.

Olivia Zvedi alikuwa akijibu katika kesi iliyoletwa na wafungwa waliohukumiwa kunyongwa ambao wanaelezea hali ya wasiwasi inayotokana na kipindi kirefu kinachochukuliwa kabla ya kutekelezwa hukumu hiyo kuwa inayokiuka katiba.

Wakili wao anasema kukaa bila hukumu kwa kipindi hicho ni kuwadhalilisha, na adabu isiyokuwa ya kibinadamu inayowapa mawazo na mateso.

Wafungwa hao wanataka hukumu ya kifo ibadilishwe na kuwa kifungo cha maisha. Mara ya mwisho mfungwa kunyongwa nchini Zimbabwe ilikuwa 2005.

Ilidhaniwa kuwa nafasi ya mnyongaji iliyokuwa wazi kwa miaka 8 ilijazwa mwaka 2013.

Lakini tangazo la leo la kiongozi wa mashtaka ni kinyume aliposema watu hawapo wa kukubali kazi hiyo. Kuna wafungwa 76 wanaosubiri kunyongwa kwa miaka 20. Mahakam ya katiba itaamua kesi hiyo baadaye.