Oparesheni ya kijeshi hotelini B Faso yakamilika

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwanajeshi akikabiliana na wavamizi wa hoteli ya Splendid nchini Burkina Faso

Oparesheni ya kuizunguka hoteli moja iliovamiwa na wapiganaji imeisha ,serikali imetangaza,lakini ripoti zinaarifu kwamba hoteli nyengine iliopo karibu imeshambuliwa.

Watu 126 waliokuwa mateka waliachiliwa huru katika hoteli ya Splendid iliopo katika mji mkuu wa taifa hilo la Magharibi mwa Afrika Ouagadougou, kwa mujibu wa waziri wa maswala ya ndani.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Magari ya kijeshi yakipiga doria nje ya hoteli ya Splendid

Wapiganaji wanne waliuawa aliongezea huku watu 23 wa mataifa 18 tofauti wakifariki wakati wa shambulio ambalo pia liliulenga mgahawa huo.

Vikosi maalum vya Ufaransa vinasaidia wanajeshi wa taifa hilo katika oparesheni hiyo.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande ameshtumu shambulio hilo la taifa hilo ambalo lilikuwa koloni yake hapo zamani.

Image caption Hali ya kawaida yarudi Burkina Faso

Kundi la Al-Qaeda la islamic Maghreb{AQIM} limesema kuwa lilitekeleza shambulio hilo katika taifa hilo la Magharibi mwa Afrika.

Mnamo mwezi Novemba shambulio la AQIM katika hoteli moja ya Bamako nchini Mali liliwauwa watu 19.