Hoteli yatekwa na wapiganaji Burkina Faso

Image caption Ramani ya eneo lililoshambuliwa

Maafisa wa usalama katika taifa la Magharibi mwa Afrika la Burkina Farso, wameanza mashambulizi kujaribu kuikomboa hoteli ambayo ilitekwa na wapiganaji Waislamu wenye itakadi kali walio na bunduki.

Mateka kadhaa wanadhaniwa kuwa katika jengo hilo katika mji mkuu wa OuagaDougou.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Maafisa wa polisi wakijiandaa kukabiliana na wapiganaji.

Makomando walitegua vilipuzi waliopanza mashambulizi hayo na kwa wakati huu sebule ya hoteli hiyo inateketea.

Inadaiwa kuwa watu kadhaa wameuawa. Mkurugenzi wa hospitali moja aliyezungumza na manusura amesema kuwa waliofariki huenda wakawa zaidi ya 20.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Maafisa wa polisi wakiowaondoa baadhi ya mateka katika hoteli ya Splendid

Kundi la wapiganaji, lenye uhusiano na Al-Qaida, limedai kuhusika katika mashambulizi hayo.

Washambulizi hao pia walivamia mgahawa mwingine uliokuwa karibu na hoteli hiyo. Taasisi hizo zinapendwa sana na wateja wa kigeni kutoka mataifa ya Magharibi.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Eneo moja la hoteli hiyo linaonekana likichomeka kufuatia mashambulizi

Mapema mchana watu wenye bunduki waliwaua watu wawili katika shambulio lililofanywa karibu na mpaka na Mali.

Haijulikani kama mashambulizi hayo yaha uhusiano wo wote na