Taiwan yamchagua rais wa kwanza mwanamke

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais mteule wa Taiwan bi Tsai Yingwen

Mgombea anayeunga mkono harakati za uhuru kwenye taifa la Taiwan Tsai Yingwen kutoka chama cha Democratic Progressive ameshinda uchaguzi wa urais nchini humo.

Chama tawala cha Kuomintang ambacho kinapendelea ushirikiano na upande wa bara wa taifa la Uchina kimepoteza uchaguzi huo.

Baada ya nusu ya kura zote kuhesabiwa mpaka sasa, chama cha DPP kimeonyesha kuongoza kwa kishindo ikiwa wana zaidi ya asilimia 60 ya kura zote zilizopigwa mpaka sasa.

Bi Tsai atakuwa rais wa kwanza mwanamke kwenye dunia ya wazungumzaji wa lugha ya Kichina. Anatarajiwa kutoa hotuba ya ushindi punde.

Mwanidishi wa BBC mjini Taipei anasema ushindi wake unaweza kuanzisha mzozo na Uchina ambayo inaitazama Taiwan kama jimbo lake muhimu.