Raia wa Taiwan wapiga kura

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Uchaguzi waendelea kisiwani Taiwan

Upigaji kura wa Bunge na urais unaendelea nchini Taiwani, swala la uhusiano kati ya eneo hilo la Uchina likipewa kipao mbele katika kampeni.

Chama kinachotawala cha KMT, kinachounga mkono kuungana kwao na Uchina - kinakabiliwa na upinzani mkali kutoka chama kinachotaka kupinga uhusiano wo wote na Uchina cha Democratic Progressive Party.

Uchina imedai kutawala eneo hilo tangu kushindwa kwa viongozi kadhaa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika mwaka 1949.

Viongozi walioshindwa walikimbia kujificha katika visiwa hivyo, huku Wakomunisti wakithibiti maeneo kadhaa.