Wanandoa watekwa Burkina Faso

Haki miliki ya picha annonymous
Image caption Splendid hoteli iliovamiwa na wapiganaji siku ya ijumaa

Idadi kubwa ya watu imeendelea kutoa risala zao kufuatia kutekwa nyara kwa wanandoa wawili wa Australia, na watu wanaoaminika kuwa wapiganaji wa Kiislamu nchini Burkina Faso.

Daktari Ken Elliot na mkewe ambao wana umri wa miaka themanini, wamejenga vituo kadhaa vya afya tangu miaka ya sabini katika mji wa Djibo karibu na mpaka wa nchi hiyo na Mali.

Wakaazi wa mji huo sasa wameanzisha mtandao maalum wa facebook, kushinikiza kuachiliwa huru kwa wawili hao.

Awali utawala wa nchi hiyo ulisema kuwa watu ishirini na tisa waliuawa baada ya wanamgmabo wa kiislamu kushambulia hoteli moja mjini Ouagadougou.