Rais wa Iran apongeza kuondolewa kwa vikwazo

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Javad Zarrif

Rais wa Iran, Hassan Rouhani, amepongeza kutekelezwa kwa mkataba uliosaniwa kuhusiana na mpango wake wa Nuklia.

Rais Rouhani amesema kuondolewa kwa vikwazo ambavyo havikustahili dhidi ya serikali yake, kumeashiria mwanzo mpya wa maendeleo wa taifa lake.

Rais huyo amehutubia bunge la nchi hiyo baada ya shirika la umoja wa mataifa kuthibitisha kuwa Iran haikuwa inatengeneza silaha za nuklia, hali iliyopelekea vikwazo dhidi yake kuondolewa.

Haki miliki ya picha
Image caption Mkutano kati ya Marekani

Rouhani amesema kile mtu amefurahia mkataba huo, isipokuwa wale aliowataja kama wachochezi wa kanda hiyo, Israel na wabunge kadhaa wenye msimamo mkali katika bunge la congress nchini Marekani.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesema, tishio la Iran kutengeneza silaha za nuklia limpunguzwa lakini amesema wataendelea kuchunguza kwa umakini.