Albamu ya David Bowie yaongoza kwa mauzo

Image caption Kumbukumbu za kumuezi david Bowie

Albamu ya Black starya gwiji wa muziki Marehemu David Bowie inaongoza kwa mauzo nchini marekani baada ya kutolewa siku mbili kabla ya kifo chake.

Albamu hiyo imeuza kopi 181,000 na hivyobasi kuipiku albamu ya Adele katika kilele cha albamu inayouza sana nchini humo.

Albamu yake iliouza sana ni ile ya The Next day ambayo ilichukua nafasi ya pili kwa mauzo mwaka 2013.

Blackstar ndio albamu ya kwanza nchini Marekani kuuza sana baada ya kifo cha aliyeitunga tangu albamu ya Michael jackson This is it ilioongoza katika mauzo mnamo mwezi Novemba mwaka 2009.

Albamu nyengine tisa za Bowie pia ziliorodheshwa miongoni mwa albamu 200 za Billboard wiki hii huku albamu ya The best of Bowie ikishika nafasi ya nne huku The Rise and Fall of Ziggy Stardust na Spiders from Mars zikishikilia nafasi ya 21.

Kibao chake cha kwanza kilivuma mwaka 1972.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Marehemu David Bowie

Kibao hicho hakikupata mafanikio makubwa na kiliorodheshwa katika nafasi ya 66 mwaka huo.

Msanii huyo alifariki mapema mwezi huu baada ya kuugua kwa miezi 18 akikabiliana na ugonjwa wa saratani.

Mashabiki duniani wamekuwa wakimuenzi mwanamuziki huyo aliyekuwa na miaka 69 katika maonyesho pamoja na maeneo ya kumbukumbu yanayohusishwa na mwanamuziki huo.