Wagombea wa Democratic wakabiliana

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Bernie Sanders na Hillary Clinton

Wagombea kupitia chama cha Democratic kwenye kinyanganyiro cha kuwania urais nchini marekani wamekabiliana kuhusu suala ya kudhibiti umiliki wa bunduki na afya katika mdahalo uliokuwa wenye msisimko uliopeperushwa kwa njia ya runinga.

Hillary Clinton alimshambulia Bernie Sanders kuhusu mipango yake la kudhidibiti umiliki wa bunduki na pia kusema kuwa mpango wake wa afya unahatarisha sheria za sasa.

Bwana Sanders naye alimlaumu Bi Clinton kwa kuegemea upande wa taasisi ambazo zilisababisha kuwepo hali ngumu ya kiuchumi mwaka 2008.

Huku Bi Clinton akiongoza kote nchini, bwana Sanders ni tisho katika majimbo makuu.

Saa chache kabla ya mdahalo huo bwana Sanders alikuwa amezindua mpango wa afya kwa raia wote wa marekani.

Aliyekuwa meya wa Maryland Martin O'Malley ambaye yuko nyuma ya Clinton na Sanders naye alishiriki katika mdahalo huo.