Katanga kufunguliwa mashtaka DRC

Haki miliki ya picha ICC
Image caption Germain Katanga alikuwa aachiliwe leo

Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo inasema kuwa inataka kumfungulia mashtaka kiongozi wa waasi Germain Katanga ambaye tayari amehukumiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC.

Katanga alikuwa akitumikia kifungo chake gerezani katika mjini Kinshaha na alikuwa aachiliwe hii leo.

Waaziri wa haki nchini DRC Alexis Thambwe Mwamba aliliamba shirika la habari la AFP kuwa Katanga hawezi kuachiliwa.

Anatakikana nchini Jamhuri wa kidemokrasi ya Congo kwa uhalifu tofauti wa kivita na ule uliotumiwa kumhukumu kwenye mahakama ya ICC.

Mwezi uliopita shirika la haki za binadamu lenye makao yake nchini Marekani lilisema kuwa Katanga anatakikana kwa uhalifu uliotendwa mwaka 2005 na kutaka kesi yake ifanyike kwa haraka.