UK kukabiliana na ubaguzi wa wanawake Waislamu

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wanawake waislamu nchini Uingereza

Serikali ya Uingereza itatoa dola milioni 22 ili kuwarai wanawake Waislamu wanaoishi katika taifa hilo kusomea lugha ya Uingereza.

Ni miongoni mwa msukumo wa kujenga jamii thabiti na kukabiliana na itikadi kali.

Akiandika katika gazeti la The Times, Waziri Mkuu David Cameron ameishtumu idadi ndogo ya wanaume waislamu kwa kuwa na fikra za zamani za kuwadhibiti makumi ya maelfu ya wanawake ambao huzungumza Kiingereza kiasi ama hata wale wasioijua lugha hiyo.

Amesema kuwa Uingereza inafaa kushinikiza kuhusu maadili yake ya kuwa huru na kwamba wanawake wanaozuru taifa hilo kwa kutumia viza ya ndoa watafanya mtihani wa lugha iwapo wanataka kuongeza mda wa kuishi ama kutuma ombi la kutafuta uraia.