Zambia yailima zimbabwe bao 1-0

Haki miliki ya picha
Image caption Kombe la Chan

Zambia imewanyuka majirani wao Zimbabwe bao moja kwa sufuri wakati wa mechi ya ufunguzi ya kundi D kwenye mechi za kuwania ubingwa wa afrika(Chan) katika mji wa Rubavu nchini Rwanda.

Isaac Chansa alifunga bao hilo la pekee mnamo dakika ya 58.

Alijivuta na kupata mkwaju wa free Kick uliochongwa na nahodha wake Chrisopher Katongo ambaye aliliinua kombe ya taifa bingwa barani afrika mwaka 2012.