Twitter yakumbwa na matatizo

Haki miliki ya picha PA
Image caption Twitter inasema kuwa ilikuwa inafahamu tatizo hilo na ilikuwa imewasiliana na wanachama wake

Mtandao wa kijamii wa twitter umekumbwa na matatizo kwa watumiaji wengi kufuatia suala la kiufundi.

Watumiaji wengi wa simu za mkononi wameshindwa kusoma au kuchapisha kwenye mtandao huo ambao una karibu wanachama milioni 300.

Twitter inasema kuwa ilikuwa inafahamu tatizo hilo na ilikuwa imewasiliana na wanachama wake.

Msemaji wa Twitter alisema kuwa ujumbe kutoka kwa kampuni hiyo ulisema."Tunakumbwa na matatizo katika kutumika kwa twitter. Tunafahamu hilo na tunalishughulikia."