Korea Kaskazini yagundua pombe isiyoleta uchovu

Image caption Watu wakishangilia nchini Korea Kaskazini

Wanasayansi nchini Korea Kaskazini wamegundua aina ya pombe ambayo haisababishi uchovu baada ya mlevi kunywa kunywaji hicho kulingana na vyombo vya habari nchini humo.

Gazeti la Pyongyang Times nchini humo linasema kuwa pombe hiyo haimletei mlevi uchovu wakati anapoamka asubuhi.

Pombe hiyo inaripotiwa kutengezwa kutoka kwa mmea mmoja wa asili unaofahamika kama insam pamoja na mchele.

Vyombo vya habari nchini Korea kaskazini vinafafahamika kwa kutangaza mambo yasiyokuya ya ukweli kuhusu mafanikio ya nchi hiyo.

Mwaka uliopita korea kaskazini ilisema kuwa madawa yanayotengenezwa kutoka kwa mmea huo wa insam yanaweza kuponya magonjwa yakiwemo Sars na virusi vya ukimwi.