Mwandishi wa BBC azuiwa kwenda Marekani

Rana Rahimpour Haki miliki ya picha Zoubin Navi
Image caption Rana Rahimpour ni mtangazaji wa BBC wa idhaa ya kiajemi

Mwandishi wa BBC journalist mwenye uraia wa chini mbili Uingereza na Iran amezuiwa kusafiri kuelekea nchini Marekani baada ya kushindwa kutimiza masharti ya sheria za visa zilizobadilika.

Rana Rahimpour aliambiwa na maafisa wa Marekani kwamba asingeweza kusafiri chini ya mfumo wa visa uliopo.

Chini ya sheria mpya, watu wenye uraia wa nchi mbili kutoka nchi kadhaa lazima watatakiwa kuomba visa katika ubalozi wa Marekani.

Lakini Bi Rahimpour alisema ushauri aliopewa kutoka ubalozi wa kuhusu ikiwa sheria zimetekelezwa haukua wa wazi.

Tovuti ya wizara ya mambo ya nje ya Uingereza inasema kuwa sheria hizo mpya kuhusu visa zitaanza kutekelezwa kuanzia tarehe 1 Aprili, huku tovuti ya Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani ikisema tayari mamlaka ''zimeanza kutekeleza mabadiliko '' ya mfumo wa utoaji visa

Haki miliki ya picha
Image caption Binamu wawili wa Rana Rahimpour pia walizuiwa kwenda Marekani

Ni pale tu alipowasiliana na shirika linaloshughulikia mfumo mpya wa utoaji visa katika uwanja wa ndege, ndipo Bi Rahimpour - mtangazaji wa Idhaa ya BBC ya Kiajemi - aliambiwa kuwa uraia wake haumruhusu kusafiri.

'haikuwa haki kwake'

Bnamu zake wawili pia walizuiwa kusafiri. Walikuwa wakitarajia kusafiri kwa ndege kutoka Heathrow kuelekea Marekani kwa ajili ya sherehe ya kuzaliwa .

Bi Rahimpour alielezea sheria mpya kama "zisizo za haki ", akibainisha namna zinavyowabanaraia wa Iran waliopta uraia kupitia ndoa ama uzazi .

Sheria hizo mpya ambazo pia zinawaathiri raia kutoka mataifa ya Iraqi, Syria na Sudan wenye uraia wa nchi mbili , zimezua hasira.