Ukosefu wa chakula waikumba CAR

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption WFP inasema kuwa watu milioni 2.5 hawana chakula

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema nusu ya watu katika nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ambao ni karibu watu milioni 2.5 hawajui penye watapata mlo wao wa siku.

WFP inasema viwango vya sasa vyka ukosefu wa chakula ni vya kutia wasiwasi.

WFP inasema kwa sababu kubwa ni kuwa wakulima hawajaenda mashamba yao kufanya kilimo kutokana na hali mbaya ya usalama nchini humo.