Makampuni ya dawa yahitaji fedha kukabiliana na vimelea

Haki miliki ya picha PA
Image caption Dawa za bacteria wasiosikia dawa

Baadhi ya makampuni mashuhuri ya utengenezaji wa dawa za tiba duniani yametowa wito kwa serikali za mataifa kutafuta njia mpya ya kuyalipa makampuni hayo ili yaweza kubuni dawa mpya za kupambana na vimelea au bacteria.

Makampuni hayo yamesema juhudi za pamoja zinahitajika kukabiliana na vimelea visivyosikia dawa ambavyo vimeibuka na kutishia maisha ya mamilioni ya watu kote duniani.

Zaidi ya makampuni mia moja ya kimataifa ya utengenezaji dawa ikiwemo kampuni ya GSK, Pfizer na Johnson & Johnson yametia saini azimio la kukabiliana na maambukizi yasiyosikia dawa.

Mpango huo unazinduliwa katika kongamano la kiuchumi duniani mjini Davos.