Mauaji ya kale yagunduliwa Turkana Kenya

Image caption Mabaki ya watuo waliofariki yapata miaka 6000 iliopita katika ziwa Turkana nchini Kenya

Wanakiolojia wamepata ushahidi kaskazini mwa Kenya katika kile huenda ni mfano wa vita kati ya jamii tofauti.

Mabaki hayo ya miaka 10,000 kutoka kwa watu 27 ambayo yalipatikana magharibi mwa Ziwa Turkana yanaonyesha kuwa yalisababishwa na mauaji.

Waliwachwa kufa katika eneo hilo badala ya kuzikwa.Wataalamu wengi walidhani mgogoro huo ulitokea yapata miaka 6000 baada ya raia kupata makaazi.

Wanakiolojia hao ambao wamekuwa wakifanya kazi katika eneo hilo la Nataruk tangu mwaka 2012,waligundua kwamba waathiriwa walichapwa ama hata kudungwa visu kwa pamoja.

Waliouawa ni wanaume na wanawake pamoja na watoto.

Ushahidi,uliochapshwa katika jarida la asili hauonyeshi kile kilichotokea lakini ni kitu kilichosababishwa na mgogoro kulingana na profesa Robert Foley wa Chuo kikuu cha Cambridge.