Kisa cha pili cha Ebola Sierra Leone

Mwanamke Haki miliki ya picha AP
Image caption Mwanamke anayeugua ni shangaziye mwanafunzi aliyefariki wiki iliyopita

Sierra Leone imethibitisha kisa cha pili cha maambukizi ya Ebola katika kipindi cha chini ya wiki moja baada ya kumalizika kwa mlipuko wa ugonjwa huo Afrika Magharibi.

Kisa hicho kipya ni cha shangaziye mwanafunzi wa umri wa miaka 22 aliyefariki kutokana na virusi hivyo wiki iliyopita.

Mwanamke huyo ndiye aliyekuwa akimtunza mwanafunzi huyo alipokuwa mgonjwa, msemaji wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tarik Jasarevic ameambia shirika la habari la AFP.

Alianza kuonyesha dalili za kuugua Jumatano akiwa katika kituo cha karantini na kwa sasa anapokea matibabu.