Ujangili wa Faru wapungua Afrika Kusini

Image caption Pembe za Faru zina soko kubwa barani Asia

Ujangili unaofanywa dhidi ya Faru unaofanywa kwa ajili ya biashara ya pembe zao nchini Afrika kusini umeshuka kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2007, maafisa wameeleza.

Kulikuwa na matukio 1,175 mwaka 2015 ikilinganishwa na 1,215 mwaka uliotangulia

kupungua huku ni kwasababu ya sera zilizowekwa na operesheni ya kupambana na ujangili.

Vitendo huvi vya uwindaji haramu vinatokana na msukumo wa biashara ya pembe katika nchi za bara la Asia

tangu mwaka 2007, baada ya faru 13 kuuawa nchini humo,idadi ya wanyama waliouawa iliongezeka kwa kasi.

Waziri wa maswala ya mazingira nchini Afrika kusini Edna Molew, amesifu hatua ya kupungua kwa vitendo vya ujangili akisema ni jitihada za serikali katika kuweka sera za kupambana na ujangili.

Hatua zilizochukuliwa kupambana na ujangili ni pamoja na kufanya uchunguzi kwenye viwanja vya Ndege na mipakani na kutumia teknolojia ya kupambana na ujangili.

Amesema kuwa majangili 317 wamekamatwa mwaka jana kwa makosa ya kuua faru.mwaka 2014 watu 258 walikamatwa.

Afrika kusini ina asilimia 80 ya faru wapatikanao duniani lakini kuna hofu kuwa huenda wakatoweka miaka 10 ijayo.