Sri Lanka kuunda mahakama ya uhalifu wa kivita

Image caption Rais wa Sri Lanka Maithripala Sirisena

Rais wa Sri Lanka amesema majaji wa kigeni na waendesha mashtaka hawapaswi kujihusisha na uchunguzi kuhusu shutuma za uhalifu wa kivita

Katika Interview na BBC Rais, Maithripala Sirisena amesema nchi yake haihitaji kuwaleta wataalam kutoka nje.

Jeshi na waasi wa Tamil Tiger wanashutumiwa kujihusisha na vitendo vya kikatili wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika mwaka 2009.

Serikali awali iliunga mkono maazimio ya Umoja wa mataifa kutaka Mahakama inayosikiliza kesi kuhusu uhalifu wa kivita kuwa na majaji wa kigeni.

Lakini siku ya Alhamisi Rais alisema ‘’ sitakubali suala hili kuingiliwa na watu kutoka nje’’

Tuna wataalam wengi, na watu wenye ufahamu nchini mwetu ambao wanaweza kutatua maswala ya ndani ya nchi yetu’’

‘’jumuia ya kimataifa haina haja ya kuwa na wasiwasi na maswala yenye maslahi na nchi yetu’’

Alipoulizwa kuhusu ni lini mahakama hiyo itaundwa alisema ni mchakato mrefu