Mazungumzo ndiyo yataleta amani Burundi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Umoja wa Mataifa unasema mazungumzo ndiyo yatatatua hali nchini Burundi

Wanadiplomaai kutoka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wamemauambia waziri wa mashauri ya kigeni nchini Burundi kuwa hali iliyopo nchini humo inaweza tu kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo.

Mamia ya watu wameuawa kwenye ghasia tangu mwezi Aprili wakati rais Pierre Nkurunziza alitangaza kuw angewania urais kwa muhula wa tatu.

Naibu balozi wa Ufaransa kwenye Umoja wa Mataifa Alexis Lamek aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa mapigano lazima yakome na mauaji pia lazima yakome.