Mariah Carey ampata mchumba

Carey Haki miliki ya picha Getty
Image caption Carey allihudhuria sherehe ya kufungua kasino ya Packer mjini Macau mwaka jana

Mwanamuziki nyota wa muziki aina ya pop Mariah Carey amempata mchumba.

BBC imefahamu kwamba mwanamuziki huyo kutoka Marekani ana uchumba na bilionea kutoka Australia James Packer.

Wawili hao walionyesha uhusiano wao hadharani Juni mwaka jana baada ya kwenda likizoni pamoja nchini Italia.

Bw Packer, 47, ndiye wa nne kwa utajiri Australia, kwa mujibu wa Forbes.

Utajiri wake unakadiriwa kuwa zaidi ya A$4.7bn ($3.1bn £2.3bn).

Mariah Carey, 45, alichomoa albamu yake ya kwanza 1990 na ni mmoja wa wanamuziki waliofanikiwa zaidi duniani.

Bw Packer aliyerithi himaya ya kibiashara ya vyombo vya habari Australia kutoka kwa babake Kerry Packer, na sasa anamiliki kasino nyingi.

Alitengana na mkewe wa pili, mwanamitindo ambaye pia ni mwanamuziki Erica Baxter, mwaka 2013.

Bi Carey alitangaza kuvunjika kwa ndoa yake na mtangazaji wa kipindi cha "America's Got Talent" Nick Cannon mwaka 2014.