Mfungwa akataa kuondoka Guantanamo

Haki miliki ya picha AP
Image caption Anataka kupelekwa nchi ambapo kuna familia yake

Mfungwa kwenye gereza la Guantanano Bay ambaye alipinga kufungwa kwake kwaakususi chakula kwa muda mrefu amechukua hatua isiyo ya kawaida kwa kukataa kundoka gereza hilo la Marekai nchini Cuba, alipokataa kupelekwa nchi mpya asiyoifahamu

Muhammad Bawazir, raia wa Yemen mwenye umri wa miaka 35 alikataa kuabiri ndege kama wafungwa wengine wawili waliokuwa wakisafirishwa kwenda mataifa ya Balkans kwa mjibu wa wakili wake.

Kutoka na sababu hangepelekwa kwao nyumbani , alisisitiza kupelekwa nchi ambapo kuna familia yake.

Wakili wake alilimbia shirika la habari la AP kuwa imechukua miezi kadha kumshawishi Bawazir kukubali kupelekwa nchi nyingine ambayo hakuitaja.

Lakini mfungwa huyo ambaye alikuwa na miaka 21 wakati alikamatwa nchini Afghanistan alikataa dakika za mwisho kuwa hangefanya hivyo.