Ugaidi:Wanajeshi kulinda hoteli nchini Senegal

Image caption Senegal

Wanajeshi wamekuwa wakiwekwa nje ya hoteli kubwa nchini Senegal ikiwa ni miongoni mwa mipango ya kukabiliana na ugaidi,waziri wa maswala ya ndani amesema.

Abdoulaye Daouda Diallo amekuwa akiweka mikakati inayochukuliwa na serikali ili kuzuia mashambulizi ya kigaidi katika mji mkuu wa Dakar.

Alikuwa akijibu maswali kutoka kwa wabunge wa Senegal walio na wasiwasi na mashambulizi ya kigaidi yanayotekelezwa katika miji ya Mali na Burkina faso.

Bwana Diallo amesema kuwa hoteli ndogo pia zimekuwa zikitembelewa na maafisa wa polisi ili kuangazia mikakati yao ya usalama.

Aliwaandikia wamiliki wa hoteli hizo kuimarisha usalama wao la sivyo zifungwe.

Utalii nchini Senegal umeathiriwa sana na ukosefu wa uthabiti katika eneo hilo pamoja na kuzuka kwa ugonjwa wa ebola.