Kunyoa ndevu ili 'kukabiliana na itikadi kali'

Haki miliki ya picha
Image caption Wanaume wanaofuga ndevu Tajikistan

"Waliniita salafi,mwenye itikadi kali na hata adui wa jamii.

''Hawakuogopa kutumia lugha chafu dhidi yangu,na baadaye wawili walinishika mikono na mwengine kunyoa ndevu zangu''.

Djovid Akramov anaelezea alivyosimamishwa na maafisa wa polisi wa Tajik nje ya nyumba yake,akiwa na mwanawe wa miaka 7 na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Dushanbe.

Alikuwa miongoni mwa maelfu ya wanaume nchini Tajikistan waliokamatwa miaka kadhaa iliopita kwa kufuga ndevu.

Baada ya kukamatwa walichukua alama zao za vidole na walinyolewa kwa lazima.

Unyoaji wa ndevu ni miongoni mwa kampeni zinazolenga mambo yanayodhaniwa kuwa mageni na yasiokubaliana na utamaduni wa Tajik.

Kampeni hiyo imeelezewa kuwa muhimu katika kukabiliana na itikadi kali,huku kukiwa na hofu kuwa eneo la Asia ya katikati inafuata utamaduni wa mataifa kama vile Afghanistan,Iraq na Syria zinazofuata itikadi kali.

Kufikia msimu wa joto ilikadiriwa kuwa kati ya watu 1500 hadi 4000 kutoka katikati ya bara Asia walijiunga na makundi tofauti ya wapiganaji nchini Syria na Iraq.

Akiripoti kuhusu maendeleo kuhusu vita dhidi ya itikadi kali,mamlaka imetangaza kwamba maafisa wa polisi waliwanyoa wanaume 13,000 katika jimbo la Khatlon mwaka uliopita.

Kampeni hiyo pia inawalenga wanaume wanaovaa hijabu.Kuna marufuku rasmi ya vazi la hijabu katika shule na vyuo vikuu,lakini sheria hiyo inatekelezwa katika taasisi zote.

''Musiabudu tamaduni za kigeni,vaeni mavazi yenye rangi za kitamaduni na munyoe.hata wakati wa maombelezi,wanawake wa Tajik huvaa nguo nyeupe na sio nyeusi'', alisema rais wa Tajik Emomali Rahmon.

Image caption Mwanamume anayefuga ndevu

Mamlaka awali ilikuwa imewataka wazazi kuwapa wana wao majina ya Tajik.

Djovid Akramov anasema kuwa hatosahau alivyofedheheka wakati alipolazimishwa kunyolewa katika kituo cha polisi.

''Ubaya zaidi ni ukatili wa polisi ambao hutumia fursa hiyo kuwanyanyasa watu'',alisema.

Anadhani kwamba hakuna haja ya kulalamika na kwamba ni mambo hayo ambayo huwafanya watu kuwa na itikadi kali.

Kulingana na data rasmi, asilimia 99 ya idadi ya waislamu wa Tajik ni waislamu.

Wengi,isipokuwa idadi ndogo ya jamii ya washia katika jimbo la Badakhshan ni wa suni.