Oscar sasa kukabiliana na madai ya ubaguzi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa tuzo hiyo Cheryl Boone Isaacs amefanya mabadiliko hayo

Waandalizi wa Tuzo za Oscar wameahidi kuwa wataimarisha juhudi zao za kuongeza wanachama zaidi wanawake na watu wa kutoka katika jamii za wachache kama vile watu weusi ifikapo mwaka 2020.

Marekebisho yamefanywa baada ya juma moja la lawama baada ya kukosa washindi weusi walioorodheshwa kutangazwa katika hafla ya shughuli hizo mwezi ujao.

Haki miliki ya picha .
Image caption Spike lee

Haki ya upigaji kura kwa wanachama pia imewekewa muda wa miaka kumi pekee.

Waigizaji na waandalizi kadha wa filamu kama vile mwigizaji Will Smith na mwandalizi mkuu Spike Lee wamesema kuwa watasusia hafla za tuzo za Oscar mwaka huu kwa kuwa wote walioteuliwa ni wazungu.