Virusi vya Zika:Waonywa kutoshika mimba Brazil

Haki miliki ya picha AP
Image caption Watoto walioathirika na Zika

Maafisa wa Afya wa Brazil wanasema kuwa wanahofia kwamba maradhi yanayoenezwa na mbu ya virusi vya Zika huenda yameenea kuliko walivyotarajia.

Virusi hivyo vimedaiwa kusababisha ongezeko la ulemavu miongoni mwa watoto wadogo wanaozaliwa nchini humo.

Hofu imetanda wakati huu ambapo mji mkuu wa Rio unatarajia kuwa mwenyeji wa michezo ya Olympiki mwaka huu.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Kukabiliana na virusi vya Zika

Watafiti wamesema kuwa hali ya hewa yenye unyevu mkubwa ndiyo iliyochangia pakubwa mlipuko wa maradhi hayo.

Kampeni ya kuwahamasisha wananchi kuyaondoa maji yaliyosimama, ambako mbu wanazaana imeanzishwa huku juhudi za kubuni chanjo zikiendelea.

Idara ya Afya nchini Marekani imewaonya wanawake waja wazito wasitembelee mataifa 20 katika eneo la Brazil, kukiwemo sehemu zingine kama vile visiwa vya Samoa na Cape Verde.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mbu wanaosababisha ugonjwa huo.

Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema kwamba karibu mataifa kumi ya Afrika, Asia na Pacific pia yametangaza mlipuko wa maradhi hayo ya Zika.