Mugabe "mzima kama kigongo"

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rais Robert Mugabe asema ni mzima kama kigongo

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amerudi nyumbani baada ya likizo ya mwezi mmoja nchi za nje, juma moja baada ya wakuu kukanusha ripoti kwamba alishikwa na ugonjwa wa moyo.

Bwana Mugabe, mwenye umri wa miaka 91, alisema ni mzima kama kigongo.

Anakutana na kiongozi mwengine mkongwe wa Afrika, Teodoro Obiang Nguema wa Equatorial Guinea, ambaye anafanya ziara rasmi nchini Zimbabwe.

Rais Nguema ameongoza Equatorial Guinea kwa miaka 36, mwaka mmoja zaidi ya Rais Mugabe.