Kijana 17, aliyeua watu 4 Canada akamatwa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kijana 17, aliyeua watu 4 Canada akamatwa

Polisi nchini Canada wamemfungulia mashtaka kijana wa miaka 17 kwa makosa manne ya mauaji.

Hatua hiyo imefuatia matukio ya kuuawa kwa kupigwa risasi kwa watu nyumbani na shuleni katika eneo moja siku ya Ijumaa.

Kijana huyo anashtakiwa kwa kujaribu kuua watu saba waliojeruhiwa kwenye shambulizi hilo.

Polisi wanasema kuwa bado hawajabaini lengo la shambulizi hilo lililotokea eneo la La Loche.

Wawili kati ya wahasiriwa wa mkasa huo walikuwa walimu huku wawili wakiwa na vijana ambao ni ndugu.