Iran kununua ndege 114 za Airbus

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Iran kununua ndege 114 za Airbus

Waziri wa uchukuzi nchini Iran anasema kuwa nchi hiyo itatia sahihi kandarasi ya kununia ndege 114 aina ya Airbus.

Abbas Akhundi alinukuliwa na vyombo vya habari nchini Iran akisema kuwa kandarasi hiyo itatiwa sahihi wakati rais Hassan Rouhani atafanya ziara nchini Ufaransa siku ya Jumatano.

Hii ni baada ya kuondolewa kwa vikwazo vya kimataifa kufuatia mpango wa nuklia wa Iran.

Naibu wa Bwana Akhundi, pia amedokeza kuwa Iran ina hamu kubwa ya kununua ndege 100 kutoka kampuni ya Marekani, Boeing.

Haki miliki ya picha Khaneh melat
Image caption Iran inauwezo mkubwa wa kifedha baada ya kuondolewa vikwazo

Hiyo inafuatia kuondoshwa kwa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran, baada ya maafikiano kuhusu udhibiti wa mradi wake wa nyuklia wa Iran.

Wakuu wa mataifa ya Magharibi na Iran, wanasema nchi hiyo itahitaji ndege kama 400 katika mwongo ujao, ili kubadilisha ndege zake zilizokuwa kongwe mno kufuatia marufuku ya miaka mingi.