Walioshambulia Paris waoneshwa

wanamgambo wa kikundi cha kigaidi cha Islamic state wameachia picha ya video inayosemekana kuonesha wanaume tisa wenye silaha ambao walifanya shambulio la kigaidi mjini Paris mwezi novemba mwaka wa jana.

Mkanda huo wa video umebainika kuonesha baadhi ya wanaume waliokuwa wakiwasimamia wafungwa na kufanya mafunzo ya kijeshi mashariki ya kati kabla ya uvamizi wa mjini Paris.Mkanda huo wenye jina la ''wauwe popote utakapokutana nao" umemalizika kwa kuonesha picha ya bunge la uingereza wakiwa wanapiga kura ya nani anaruhusiwa kufanya mashambulizi ya anga ili kuiangamiza IS huko Syria .

Hata hivyo watu tisa waliofanya uvamizi huko Paris waliuwawa ndani ya shambulio hilo au muda mfupi baada ya uvamizi wakati watuhumiwa wengine wawili bado wanatafutwa.