Hofu ugonjwa wa MERS kuenea Thailand

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Hofu ugonjwa wa MERS kuenea Thailand

Maafisa wa afya wa Thailand, wanajaribu kuwatafuta watu kadha ambao wamekaribiana na mzee mmoja kutoka Oman, ambaye baada ya kukaguliwa, alionekana ana virusi vya ugonjwa wa mapafu wa Mashariki ya kati, MERS.

Mzee huyo wa miaka 71, aliwasili Bangkok Ijumaa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Hicho ni kisa cha pili cha ugonjwa wa MERS nchini Thailand.

Wizara ya Afya nchini humo, imesema watu 37, pamoja na mtoto wa bwana huyo aliyesafiri naye wako katika hatari ya kuambukizwa virusi hivyo.

Hicho ni kisa cha pili cha ugonjwa wa MERS nchini Thailand.