Theluji yaathiri maisha Marekani

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Furaha ya Theluji raia wa Marekani wakiruka juu!

Hali imeanza kureja taratibu katika miji ya Mashariki nchini Marekani kufuatia kuanguka theluji kubwa kuwahi kutokea katika miongo kadhaa iliyopita.

Kuna taarifa zaidi ya watu ishirini wamefariki kutoka na hali mbaya ya hewa iliyotokana na theluji hiyo.Vituo vya dharura vya kuhudumia wagonjwa vimefunguliwa kuwahudumia watu wanaopata matatizo ya mshutuko wa moyo na kuvunjika mifupa.

Gavana wa jimbo la New York Adrew amewaonya madereva kutoendesha ovyo labda pale kuwepo penye umuhimu.Amesema amri ya kutosafiri iliyotangazwa hapo awali imeondolewa na viwanja vya ndege vimefunguliwa..

"Marufuku ya kusafiri imeondolewa. Hiyo haina maana watu watoke nje na kuendesha baiskeli na kuangalia hali ilivyo. Barabara zimesafishwa katika maeneo mengi. Kuna milindiko ya theluji kwenye barabara za kuingia na kutokea ambazo bado hazijasafishwa.

Bado kuna hali ambapo magari yanaweza kukwama kwa barabarani. Hivyo tusitafsri vibaya marufuku ya kutosafiri Viwanja vya ndege vimefunguliwa. Na Mamlaka ya viwanja vya ndege imefanya kazi kubwa kusafisha viwanja vya ndege. Na sasa vipo tayari kwa ndege zitakazofanya safari."

Katika mji wa Philadephia mtu mmoja alikuwa akimsaidia jirani yake kuondoa theluji.

"Wanasaidia wetu wengine, wametusaidia na tunawasaida wengine. Mkono mmoja unaosha na mwingine unasaidia, Nimewaona watu wamekwama wanahitaji msaada, hawawezi kutoka nje na chepe zao zimevunjika kwa hiyo nimekwenda kwenye nyumba zao na chepe langu kuwasaidia.")

Si marekani pekee theluji hiyo imendoka katika nchi nyingine za Asia kama vile Korea kusini, China ,Japan na Hong Kong.