Syria yakomboa mji wa mwisho wa waasi Latakia

Haki miliki ya picha AP
Image caption Syria yakomboa mji wa mwisho wa waasi Latakia

Vyombo vya habari vya serikali nchini Syria vimeutaka mji wa Rabiya ambao ni mji wa mwisho uliokuwa unashikiliwa na waaasi katika mkoa wa pwani wa Latakia.

Shirila la wanaharakati lenye makao yake nchini Uingereza linasema kuwa hatua hiyo ilifikiwa kufuatia msaada mashambulizi ya angani ya ndege za Urusi.

Kutekwa kwa Rabiya kutairuhusu serikali ya Syria kuweka shinikizo zaidi na kuziba mitandao ya wasi kwenda Kaskazini karibu mpaka na Uturuki.

Wakati huohuo, Waziri wa mashauri ya kigeni nchini Marekani, John Kerry amesema ana matumaini kuwa mazungumzo ya amani kuhusu Syria yataanza nchini Uswisi wiki hii.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri wa mashauri ya kigeni nchini Marekani, John Kerry amesema ana matumaini kuwa mazungumzo ya amani kuhusu Syria yataanza

Bwana Kerry alisema kuwa alikuwa amezungumzia njia za kumaliza mzozo huo wakati alipofanya ziara nchiniSaudi Arabia.

Bwana Kerry amekuwa kwenye mazungumzo na waziri wa masuala ya nchi za kigeni wa Urusi Sergei Lavrov, kujaribu kukubaliana kuhusu ni kundi lipi la waasi litajiunga kwenye meza ya mazungumzo yanayoijumuisha serikali ya Syria na washirika wake Iran na Urusi pamoja na Saudi Arabia.

Mapigano yanaendelea nchini Syria huku watu 40 wakiripotiwa kuuawa katika mkoa wa Deir al-Zor kufuatia ya kile kinachoamika kuwa mashambulizi ya ndege za Urusi.