Marufuku ya usafiri Marekani imeondolewa

Image caption Amri iliyopiga marufuku safari zote mjini New York wakati wa dhoruba kali ya theluji katika mwambao wa Mashariki wa Marekani, imeondoshwa.

Amri iliyopiga marufuku safari zote mjini New York wakati wa dhoruba kali ya theluji katika mwambao wa Mashariki wa Marekani, imeondoshwa.

Madereva walikaidi amri juu ya hatari na kutozwa faini na hata wengine kukamatwa.

Hata hivo, meya wa mji, Bill de Blasio, aliwasihi watu wajiepushe na safari zisokuwa za lazima, na wabaki ndani majumbani mwao.

Watu kama 18 wamekufa katika mmiminiko wa theluji na upepo mkali.

Malaki ya watu wamekosa umeme, na ndege chache tu zinatarajiwa kuondoka New York au Washington leo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kiwango hiki cha theluji hakijashuhudiwa kwa miongo kadhaa

Maduka na majumba ya sinema yote yamefungwa huku ratiba ya mechi nyingi za michezo zikipigwa marufuku.

Maeneo makubwa ya mashariki mwa Marekani yamefukiwa na theluji .

Haki miliki ya picha b
Image caption Zaidi ya watu milioni 80 katika majimbo 18 wameathirika.

Zaidi ya watu milioni 80 katika majimbo 18 wameathirika.

Sasa usafiri wa reli na ndege uliokuwa umetatizwa umefunguliwa.

Zaidi ya watu 200,000 walibakia bila umeme.

Maeneo mengine yalishuhudia theluji yenye hadi urefu wa mita moja.