Al Shabaab: Mwandishi akamatwa Kenya

Image caption Mwandishi wa upekuzi Kenya,Yassin Juma amekamatwa na polisi

Mwandishi mashuhuri wa habari za upekuzi nchini Kenya, amekamatwa na polisi kwa kuchapisha picha za shambulizi la kigaidi dhidi ya majeshi ya Kenya nchni Somalia.

Yassin Juma anatuhumiwa kwa kuchapisha picha za Al Shabaab zikionyesha kuchomwa kwa magari ya kijeshi.

Utawala nchini Kenya umewaonya wakenya dhidi ya kusambaza picha zilizochapishwa na Al Shabaab baada ya kuwashambulia na kuua idadi kubwa ya wanajeshi.

Image caption Waziri wa usalama wa ndani nchini Kenya alionya kuwa picha hizo zinahujumu usalama wa taifa.

Waziri wa usalama wa ndani nchini Kenya alionya kuwa picha hizo zinahujumu usalama wa taifa.

Al Shabaab wanasema kuwa waliwaua zaidi ya wanajeshi 100 wa kenya lakini hilo halijathibitishwa.

Image caption Wakenya wanaishinikiza serikali imwachilie huru mwandishi huyo wa habari

Habari za kukamatwa kwake zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuibua hamaki miongoni mwa wakenya.

Yamkini, #KOT walijitokeza kwa wingi kwenya mitandao ya kijamii na kuitaka serikali imuachilie huru mwandishi huyo chini ya kibwagizo cha #FreeYassinJuma.

Image caption Kibwagizo hicho #FreeYassinJuma kinazidi kusambazwa na kufikia tulipochapisha habari hii

Kibwagizo hicho #FreeYassinJuma kinazidi kusambazwa na kufikia tulipochapisha habari hii ndio kibwagizo maarufu zaidi nchini Kenya.