Bomu laua 25 katika shambulizi Cameroon

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bomu laua 25 katika shambulizi Cameroon

Takriban washambuliaji watatu wa kujitolea mhanga wametekeleza mashambulizi katika mji ulioko Kaskazini mwa Cameroon karibu na mpaka na Nigeria.

Afisa mmoja wa serikali alisema kuwa takriban watu 25 waliuawa wengi wao wakiwa sokoni.

Kundi la wanagambo la Boko Haram linashukiwa kutekeleza mashambulizi hayo katika mji wa Bodo.

Haki miliki ya picha
Image caption Cameroon huchangia wanajeshi kwenye kikosi kilichobuniwa cha kikanda cha kupambana na Boko Haram

Mwezi uliopita washambuliaji wawili wa kujitolea mhanga wa kike walijilipua mjini humo.

Cameroon huchangia wanajeshi kwenye kikosi kilichobuniwa cha kikanda cha kupambana na Boko Haram ambao wamefanya mashambulizi mengi na kuteka maeneo mengi ya Kaskazini mwa Nigeria.