Wakimbizi: Ugiriki mashakani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wakimbizi: Ugiriki mashakani

Mawaziri wa nchi za muungano wa ulaya wanafanya mazungumzo kuhusu njia za kukabiliana na suala la wakimbizi na wahamiaji.

Zaidi ya watu milioni moja waliwasili barani ulaya mwaka uliopita hali ambayo imekuwa mzigo kwa mkataba wa ulaya (Schengen) unaoruhusu usafiri baina ya nchi za ulaya.

Kumekuwa na wito wa kuondolewa kwa muda kwa makubaliano hayo huku onyo likitolewa kuwa hatua hiyo itahujumu moja ya nguzo za muungano wa Ulaya.

Wengi wa wahamiaji huwasili kupitia nchini Ugiriki na kumekuwa na wito wa kutaka itengwe kutoka kwa kanda ya Schengen ikiwa haitadhibiti mipaka yake.

Asili mia kubwa ya wahamiaji hupitia Ugiriki wakitokea Uturuki jambo ambalo limeiudhi sana muungano wa Ulaya.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Austria imeonya kuwa huenda ikawasilisha ombi la kuitimua Ugiriki kutoka kwenye muungano huo kwa kushindwa kudhibiti mipaka yake.

Afisa anayesimamia maswala ya kigeni wa umoja wa ulaya bi Federica Mogherini, ameomba mataifa ya muungano wa Ulaya kuisaidia zaidi Ankara kukabiliana na mzigo mkubwa wa wakimbizi.

Austria imeonya kuwa huenda ikawasilisha ombi la kuitimua Ugiriki kutoka kwenye muungano huo kwa kushindwa kudhibiti mipaka yake.

Mswada huo umeungwa mkono na Ubelgiji.