UN yaunda kikosi cha amani Colombia

Image caption UN yaunda kikosi cha amani Colombia

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha kuundwa kwa kikosi kisichokuwa na silaha cha kulinda amani nchini Colombia ili kuchunguza mpango wa amani kati ya waasi wa FARC na serikali wataafikiana mkataba wa amani.

Kikosi hicho kitakua na muda wa mwaka mmoja nchini humo ikiwa ni ombi kutoka kwa pande za serikali na waasi.

Rais wa Colombia Juan Manuel Santos amesema hatua ya sasa imeifanya Colombia kuwa na tumaini la amani kwa dunia.

Mazungumzo ya amani yamekua yakifanyika nchini Cuba kwa muda wa miaka mitatu sasa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mazungumzo ya amani yamekua yakifanyika nchini Cuba kwa muda wa miaka mitatu sasa.

Mazungumzo hayo yananuiya kumaliza vita vya nusu karne ambavyo vimesababisha mamilioni ya watu kukimbia makwao.

Watu laki mbili waliuawa.

Rais Santos ameweka Machi 23 kama tarehe ya mwisho wa kusaini mkataba wa amani.